About Mama Mahanjumati
I really enjoy cooking.. : A true, personal story from the experience, I Like to Cook. Cooking can be really relaxing and fun, except for when I'm hungry.
Mama Larvene
Mama Larvene
Archive
-
▼
2010
(15)
-
▼
August
(12)
- Wali wa hoho
- Jinsi ya kupika kisamvu bila nazi
- Mapishi ya Chicken Curry
- Mapishi – Fish Finger
- Mapishi – Mayai Mchanganyiko, Tosti na Soseji
- Mapishi – Saladi ya Matunda
- Mapishi – Kisamvu cha Karanga
- Mapishi – Ndizi Mshare na Nyama
- Mapishi – Kababu (Meat Ball)
- Bajia za Dengu
- Mapishi – King Fish wa Kukaanga
- Mapishi – Mchemsho wa Samaki
-
▼
August
(12)
Thursday, August 12, 2010
Bajia za Dengu
Published :
2:41 AM
Author :
Amina Design
Kuna msomaji ameomba mapishi ya bajia hivyo leo tutaangalia mapishi ya bajia za dengu.
Mahitaji
Unga wa dengu kikombe kimoja
Vitunguu maji 2 (Katakata vipande vidogo vidogo)
Vitunguu saumu vilivyo sagwa kijiko cha chai 1
Baking Powder kijiko cha chai 1
Maji Kiasi
Chumvi
Mafuta ya kukaangia
Pilipili , Kotmiri ukipenda
Matayarisho
1. Kwenye bakuli kubwa changanya unga wa dengu na vitunguu maji na vikisha changanyika weka vitunguu saumu, kotmiri iliyokatwa katwa na baking powder. Weka chumvi kiasi kidogo.
2. Weka maji kidogo kidogo hadi mchanganyiko wako uwe mzito kisha uache kwa muda.
3. Bandika kikaango jikoni na weka mafuta, yakishachemka chota mchanganyiko wako kwa kijiko na kuweka kwenye mafuta. Angalia usiweke mara nyingi sana ili bagia zisijeshikana.
4. Zikiiva na kuanza kubadilika rangi epua na uweke mahali zitoke mafuta. Hakikisha moto sio mkali sana ili ziive na sio kubabuka.
5. Andaa tayari kwa kula na kinywaji chochote.
Enjoy!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Asante. Nimepata furusaa
ReplyDeleteInapendeza
ReplyDeleteShukran ukhty kwa mapishi murua
ReplyDelete