Biriani ni miongoni mwa vyakula ambavyo ni nadra sana kupikwa katika familia nyingi tofauti na vyakula vingine. Inawezekana ni kutokana na watu wengi kutoelewa namna ya kuoika chakula hiki kutokana na kuhitaji viungo vingi ambavyo huwapa usumbufu wapishi.
Kuna aina mbalimbali za upishi wa biriani ambapo mara nyingi hutofautiana kutokana na viungo vinavyotumika katika upishi.
Biriani la mbogamboga ni miongoni mwa aina hizo za upishi. Chakula hiki kinaweza kuliwa na kila mtu hususan wale wasiotumia nyama wala samaki.
Mahitaji:
- ½ kg mchele wa basmati
- Kitunguu maji kikubwa 1
- Nyanya 1 kubwa
- Karoti 1 kubwa
- Njegere robo kikombe
- Kiazi ulaya 1 kikubwa
- Tangawizi za kusaga kijiko 1
- Kitunguu swaumu cha kusaga kijiko 1
- Karafuu kijiko 1
- Majani ya kotimili fungu 1
- Maziwa ya mtingi ¼ kikombe
- Chumvi na pilipili kiasi
- Unga wa dhani kijiko 1 cha mezani
- Juisi ya limao kijiko 1 cha mezani
- Mafua ¼ lita
Maandalizi:
- Chemsha mchele na kisha weka pembeni
- Osha mbogamboga zote isipokuwa vitunguu na nyanya
- Changanya mtindi na tangawizi pamoja na kitunguu swaumu viache vikae kwa muda wa saa moja
- Chukua sufuria weka mafuta na kisha kaanga vitunguu maji, weka nyanya, chumvi, kotimili na limao halafu weka karafuu na kanga hadi vichanganyike vizuri
- Miminia mchanganyiko wa mtindi na baadaye weka pilipili na baadaye weka unga wa dhania
- Chukua mchele uliochemshwa changanya na mchanganyiko huo
- Palia moto juu ya chakula chako na acha kwa muda wa dakika 30
- Baada ya hapo chakula chako cha biriani kitakuwa tayari kwa kuliwa
0 comments:
Post a Comment